Na Ndetaniswa Pallangyo
Kocha Mkuu
wa Ujerumani, Joachim Loew alitumia karibu dakika nzima akizungumza na
kumpongeza beki Marcos Rojo wa Argentina.
Loew ambaye
ameipa Ujerumani ubingwa wa dunia kwa kuifunga Argentina bao 1-0 nchini Brazil,
hivi karibuni, alionekana kufurahishwa na Rojo katika mechi hiyo ya kirafiki.
Kocha huyo
alimpa mkono Rojo aliyejiunga na Man United na kuzungumza naye maneno kadhaa
huku akiutingisha mkono wake.
Katika mechi
hiyo ya kirafiki, Ujerumani ililala kwa mabao 4-2.
No comments:
Post a Comment