Sunday, 10 August 2014

AJTC yaja na wazo kufungua TV



Kushoto ni Bwana Kitomari akizungumza na mwanahabari
Mkuu wa kituo cha runinga katika chuo cha uandishi wa habari  na utangazaji arusha ajtc bwana Godlisten kitomari amesema mwitikio wa wanafunzi unazidi kuwa mkubwa huku wakifanya vizuri.

Bwana kitomari amesema wanafunzi kwa sasa wanajitahidi kufanya vipindi kama runinga kubwa nyingine nchini.

Pamoja na wanafunzi kufanya vizuri lakini pia ametaja kuwa  wanafunzi wanafanya ushindani wa vipindi kwa madarasa huku wakifuatilia kwa ukaribu mifumo ya vipindi katika runinga nyinginezo kubwa ndani na nje ya nchi.
Amesema Kufuatia mashindano hayo madarasa baadhi kama mount udzungwa yamejikuta yakifanya vizuri kupita madarasa mengine kitu ambacho kinaweza kuleta changamoto kwa madarasa mengine.

Bwana kitomari amesema kuwa juhudi hizo zinakuja kuafuatia kanuni na taratibu za kuondoa darasa linaloshindwa kufanya vipindi kwenye ratiba ya chuo.

Aidha amesema kuwa kuna mikakati ya kuikuza runinga iweze kurusha matangazo katika mikoa mbalimbali kitu kitakacho wafanya wanafunzi kuwa na mwitikio mkubwa na kupata soko sehemu nyingi.

Katika hili amesema kuwa mkuu wa chuo  Bwana Joseph Mayagila anawasaidia katika kuhakikisha mchakato huo unafanikiwa vizuri.

Hatahivyo bwana kitomari amesema wakufunzi wa chuo hicho nao wako bega kwa bega katika kuboresha mafunzo ya runinga licha ya kuwepo changamoto mbalimbali kama upungufu wa vifaa na vyumba vya mahususi katika mchakato wa urushaji wa matangazo ya runinga.

Mwandishi
Aduss Wangwe
 www.irundemtumwire.blogspot.com

No comments:

Post a Comment