Wakufunzi wa chuo cha Ajtc wakirekodi vipindi |
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotokana na uwepo wa studio za
kurekodi vipindi chuoni hapo
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha kurekodi vipindi
vya redio bwana Elihuruma Chao ambaye pia ni mkufunzi wa chuo hicho wakati
akizungumza na mwanahabari wa blog hii.
Bwana Chao amesema mwitikio wa wanafunzi katika fursa ya kujifunza
masuala ya kurekodi ni mkubwa lakini wanapaswa kuongeza juhudi zaidi ili
kufikia malengo yao ya kuwa waandishi wa habari na watangazaji bora na kuhimili
ushindani katika soko la ajira nchini na hata nje ya nchi.
Amesema suala la changamoto siyo la kuepukika katika kila
jambo hivyo wanafunzi wanapaswa kutia juhudi katika kujifunza kurekodi vipindi
kwa kutumia vifaa vilivyopo badala ya kuacha kujifunza kwa visingizio vya uhaba
wa vifaa vya kujifunzia.
Bwana Chao amesema mabadiliko ya kuhama kutoka analojia
kwenda digitali ni sawa na marudio katika chuo cha uandishi wa habari na
utangazaji Arusha kwani wao walishaanza kuwafundisha wanafunzi wao matumizi ya
vifaa vya uandishi wa habari na utangazaji kabla ya mabadiliko hayo.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi katika chuo hicho bi
Clementina Abdalah amesema uwepo wa studio za kurekodi vipindi chuoni hapo umewasaidia
wanafunzi kuwa na ujuzi wa kutengeneza vipindi bora
mmoja wa wanafunzi wa chuo cha Ajtc Arusha |
Amesema mwitikio wa wanafunzi katika kuchangamkia fursa za
kutumia studio za kurekodi vipindi ili kuimarisha ujuzi wa kutengeneza vipindi
bora vyenye kulenga maslahi kwa umma unaridhisha kwa kiasi chake ila wanapaswa
kuongeza juhudi zaidi.
Aidha chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha
kimejizolea sifa za kuwa chuo bora katika nafasi ya pili kati ya vyuo vingine
nane vya habari nchini mara baada ya kufanyika ukaguzi wa wa mwaka jana uliofanywa
na MCT na NACTE.
Viwango hivi vya habari nchini vilitangazwa mwishoni mwa
mwaka jana jijini Dar es salaam na
katibu mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga
wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari.
mwandishi
Fedinand Irunde
No comments:
Post a Comment