Na Ndetaniswa Pallangyo
NAHODHA wa
England, Wayne Rooney ameitendea haki beji katika mchezo wake wa kwanza tangu
arithi mikoba ya Steven Gerrard aliyestaafu, baada ya kufunga bao pekee katika
ushindi wa 1-0 dhidi ya Norway Uwanja wa Wembley usiku huu.
Nahodha babu kubwa; Wayne Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao pekee usiku huu
Nahodha huyo
wa Manchester United pia, alifunga bao hilo pekee kwa mkwaju wa penalti dakika
ya 68, kufuatia nyota wa Liverpool, Raheem Sterling kuchezewa rafu kwenye eneo
la penalti.
Katika
mchezo huo uliohudhuriwa na watu 40,181 – idadi ndogo zaidi ya mahudhurio
kwenye Uwanja wa Wembley tangu ufunguliwe tena, kinda Sterling alizawadiwa
heshima ya mchezaji bora mechi baada ya kazi nzuri kwenye kikosi cha Roy
Hodgson usiku huu.
No comments:
Post a Comment