Tuesday, 9 September 2014

BEI YA MBUZI YAWA CHANGAMOTO KATIKA SOKO LA MOROMBO

MWANDISHI:  EMMANUEL  MASSAWE


Wafanyabiashara wa soko la kwa morombo jijin Arusha wameulalamikia uongozi wa manispaa kwa kuwatoza kodi kubwa kulinganisha na  biashara zao

Wafanyabiashara hao ambao ni wauzaji wa mbuzi wameulalamikia mamlaka husika kuwa wamekuwa wakiwatoza ushuru mkubwa pamoja na kero ya kubadilishiwa uongozi mara kwa mara Kitendo ambacho kinapelekea wafanya biashara hao kutokuwa na imani na uongozi wa sokoni hapo


Mwandishi wa habari Emanueli Massawe akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara wa mbuzi Bwana Emanueli Kivuyo kwenye soko la kwamuorombo jijini Arusha .Picha na Jackline Malecela




Wakizungumza na mwandishi wetu mmoja wa wauzaji wa mbuzi bwana Emmanuel Kivuyo amesema kuwa wamekuwa wakitozwa elfu moja kwa kila mbuzi mmoja

“Apa tumekuwa tukitozwa bei kubwa ya ushuru kwa kila mbuzi ukilinganisha bei tunayonunulia na tunayokuja kuuzia hapa sokoni, yaani hata kama umekuja na mbuzi mia tano hapa unaweza usiuze hata moja lakini kwa upande wa ushuru lazima ulipe hata kama aujauza” alisema Emmanuel

Kwa upande wa changamoto wanazo kumbana nazo ni pamoja na kushindwa kuwatambua viongozi wa kudumu wa kutoza ushuru sokoni hapo

Bei ya mbuzi mmoja uanzia shilingi laki moja mpaka laki moja na nusu kwa mbuzi mmoja, hivyo inawafanya kuongeza bei hiyo hadi kufikia kiasi cha shilingi laki mbili hadi na nusu.

“Biashara ya mbuzi kwa sasa  imekuwa ngumu sana kutokana na ufinyu wa wateja hapa sokoni , pia kipindi ambacho mbuzi ununuliwa kwa wingi ni siku za sikukuu” aliendelea kusema Emmanuel

Alipoulizwa je kama kuna kero ambayo huwa wanakumbana nazo sokoni hapo wakiwa wanauza mbuzi katika mnada,


Picha ya mbuzi wakiwa kwenye soko la kwa muorombo jijini Arusha tayari kwa mnada wa kuunzwa.Picha na Jackline Malecela

tunasumbuliwa na madalali wanaokuja katika soko hilo kwa hajili ya kujipatia wateja pili wanawasumbua sana wateja wetu wanaokujaga kuchukuwa mbuzi hapa na pia wanawauzia bei tofauti na ya kawaida kwa kawaida mbuzi huuzwa kuanzia laki moja mpaka laki moja na nusu lakini madalali hao upandisha mpaka laki mbili na zaidi”,alisema Emmanuel

Na jitihada za gazeti hili kumpata muhusika wa kitengo cha ukusanywaji wa ushuru katika soko hilo ziligonga mwamba baada ya muhusika kukimbia alipo muona mwandishi, pia bado tunaendelea na jitihada za kumpata mtoza ushuru huyo

Akitoa wito kwa uongozi wa soko hilo kwa niaba ya wauzaji wa mbuzi bwana Emmanuel alitoa kauli ya kuwaomba uongozi kusimamia swala zima la utozwaji wa ushuru pamoja na kuakikisha wanawatoa watu wanaojiita madalali katika soko hilo pia na kuweka sheria kali kwa yoyote atakae kiuka taratibu za soko hilo.


No comments:

Post a Comment