Na Ndetaniswa Pallangyo
WAKONGWE Miroslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker
wamepewa tuzo za heshima usiku huu kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya
Ujerumani na Argentina Uwanja wa Esprit Arena.
Watatu hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la
Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani
kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi
zaidi katika ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment