Thursday, 22 May 2014

CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA CHAPATA MAKAMU MKUU WA CHUO!!

Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw Elifuraha Samboto akiteta jambo na Mkufunzi wa Nidhamu Bw Christian Ndege.
Mwalimu Elihuruma chao akiwa darasani na wanafunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji



Baadhi ya wanafunzi wa ngazi ya Cheti katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakishiriki mazoezi ya vitendo kwenye Studio yakuhariri vipindi vya Redio.
Mwalimu Elihuruma chao akiwa darasani na wanafunzi wa Darasa la Serengeti katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji



Katika  kubadilisha vipaji kwa Waadhiri tofauti Chuo cha Uandishi na Habari na Utangazaji Arusha kimefanya marekebisho ya uongozi wa ngazi za juu.
 
Akielezea mabadiliko hayo Muadhiri mlezi wa chuo hicho Bw Andrea Ngobole ametaja nafasi ambazo zimefanyiwa marekebisho ni pamoja na nafasi ya makamu mkuu wa chuo na mwalimu wa taaluma .

Bw Ngobole alimtambulisha makamu mkuu wa chuo hicho kuwa ni Bw ELIFURAHA SAMBOTO aliyekuwa mkufunzi wa taaluma  hapo awali kabla yakupandishwa cheo,  Bw ADSON KAGIYE alipewa cheo cha Mkufunzi wa taaluma kwa ngazi ya Stashahada na cheti.

Akiongea na wanafunzi wa Chuo hicho mara baada ya kutambulishwa rasmi Bw ELIFURAHA alisema ‘ninafuraha sana kupandishwa cheo japokuwa kuna changamoto nyingi zitakazonikabili wakati nikiwa natumikia nafasi hii’’
 Wapo wataonichukia sana kipindi cha utendaji haswa wale wote wasiolipa ADA kwa wakati, watoro na pia wale wasikuwa na tabia zinazofanana na za Waandishi au na Chuo hiki’’Alimalizia Bw Samboto.

Aidha aliendelea kwakusema kuwa ataitumia nafasi aliyopewa kuhakikisha kuwa anarekebisha kasoro mbalimbali zilizokuwepo hapo awali zikiwepo utovu wa nidhamu,utoro pamoja na ulevi.

Sanjari na hayo alisema kuwa atahakikisha kiwango cha taaluma kimepanda kwakuhakikisha waalimu wanakuwa madarasani wakati wote wa vipindi pia wanafunzi wanafanya mazoezi kwa njia ya vitendo kwenye Redio na televishen.

Kwa upande wa mwanafunzi  wa chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha aliyeljitambulisha kwa jina  Rachel Richard amesema yeye amefurahishwa  na mabadiliko yaliyofanyika ya uongozi kwani yapo mambo mengi yatakayoshugulikiwa ikiwepo ile ya nidhamu kwa wanafunzi.

Hata hivyo Bi Rachel amewataka wanafunzi wenzake wawe wanazingatia mda wa masomo pia wawe na nidhamu nzuri kwa wanafunzi wenzao na  hata kwa walimu kwa ujumla .

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha kilikuwa hakina makamu mkuu wa chuo kwa muda mrefu  jambo lililokuwa linapelekea kuwepo na kasoro mbalimbali zikiwepo upungufu wa madarasa,nidhamu chafu kwa wanafunzi jambo ambalo hadi hivi sasa makamu huyo ameweza kurekebisha.

HABARI NA: Rachel Lairumbe
Picha na: Maktaba




No comments:

Post a Comment