Wednesday, 10 September 2014

WAFANYABIASHARA WA MBUZI KWA MUROMBO JIJINI ARUSHA WAMEIOMBA SERIKALI KUWABORESHEA ENEO LA SOKO IKIWEMO VYOO.......

   Mbuzi wakiwa eneo la soko tayari kwa kuuzwa katika mji mdogo wa kwa Murombo jijini          Arusha..picha na EDINA LUCUS
Mwandishi wa Habari wa Ruwenzori blog Kushoto,Akisalimiana na mfanyabiashara maarufu wa mbuzi Richard Kivuyo kulia katika eneo la soko la mbuzi kwa Murombo jijini Arusha..picha na EDINA LUCUS.

Habari na KUNDAEL PHILLIP
Mkoa wa Arusha eneo la kwa murombo ni maarufu sana kwa biashara ya mbuzi kwa ajili ya matumizi ya nyama za kuchoma pamoja na supu.Biashara ya mbuzi ni maarufu sana kwa kabila la wamasai na hufanyika mara mbili kwa wiki katka soko la kwa murombo,siku ya Jumatatu na Ijumaa.

Bwana Richard Kivuyo ambaye ni mfanya biashara mkubwa na mzoefu katika soko hilo la mbuzi alisema biashara hiyo inafaida kiasi kwani hali ya uchumi kwa sasa ni ngumu ukilinganisha na kipindi cha nyuma kwani mbuzi mmoja kwa sasa ni shilingi laki moja japo msimu wa sikukuu biashara huwa nzuri kiasi unaweza ukauza kwa laki na hamsini elfu.

Biashara yetu mara nyingi tunafanyia hapahapa katika eneo la kwa murombo japo sisi tunawatoa maeneo ya vijijini huko tunapoishi na wateja wetu ni wa eneo hili japo wapo wanaotoka maeneo mengine ambao hununua kwa jili ya kitoweo na kufuga.

Aliendelea kueleza kwamba biashara hii pia ina hasara na ndio changamoto wanayokabiliana nayo inapotokea mbuzi kuumwa na kukosa tiba kwa haraka,vilevile inapotokea mbuzi akiwa mjamzito kwani tuna mbuzi jike na dume hivyo  na unapofika mda wa kuzaa inaweza kutokea mtoto akafa au wote kwa pamoja,na ukame pia huchangia kwani wakati mwingine tunalazimika kununua majani kwa sababu hayaonekani kwa urahisi.

Aliomba serikali iweze kuwasaidia kujenge soko maalumu katika eneo hili la kwa murombo kwa jili ya biashara hiyo kwani wanapofanyia biashara yao kwa sasa mazingira yake ni magumu hinyo inapofika kipindi cha mvua tope hujaa eneo hilo na biashara kuwa ngumu vilevile inapofika mda wa kiangazi nao inakua kero kutokana na jua kua kali.

 Huduma muhimu kama vyoo hakuna eneo hili inatulazimu kutoa fedha na kwenda kwenye vyoo vya kulipia ambavyo inakua vigumu wote kufanya hivyo nakua chanzo cha uchafuzi wa mazingira kwani watu hujisaidia hovyo katka eneo hili.
      ‘Hakuna vyoo kabisa katika eneo hili la biashara nayo serikali ituangalie.’alisema bwana        Richard kivuyo..








No comments:

Post a Comment