Wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wameaswa kujishugulisha na mazoezi ya vitendo pamoja kuhudhuria darasani kwa wakati ili kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa Taaluma ya Uhandishi wa habari na Utangazaji Bwana Adson Kagiye wakati alipokuwa akiongea na mwanandishi wa habari ofisini kwake hivi leo.
''Wanafunzi walio wengi hawafanyi vizuri katika masomo yao jambo linalopelekea kufeli mitihani yao nakupata madaraja ya hali chini jambo linalopelekea kutopata cheti kizuri'' alisema Bw Kagie.
Aidha ameendelea kwakusema kuwa Chuo kinao waalim Waliobobea katika taaluma mbalimbali ikwemo ya uandishi wa Habari na utangazaji pamoja na ualimu wa shule za awali na ile ya secretari
Pia ameongeza kuwa Chuo kina studio nzuri na za kisasa za kurekodia vipindi vya Redio na Televishion hali ambayo itawafanya Wanafunzi hao kuwa na uzoefu katika usomaji wa habari pamoja na vipindi mbalimbali vya Redio na Televishen.
Vilevile amesema kuwa kutokana na Wanafunzi kutofahamu vizuri Lugha ya kiingereza kumechangia pia kutokufanya vizuri katika mitihani yao hivyo amajipanga kuleta waalimu kwa ajili ya mafunzo ya muda kwa Lugha ya Kingereza.
Pamoja na hayo ameendelea kwa kusema kuwa wanafunzi ambao awajatimiza alama za kujiunga na chuo hicho watapewa kozi ya mda mfupia ya miezi kadhaa na ndipo watakapo jiunga na fani ya Uandishi wa Habari chuoni hapo.
Nae mmoja wa wanafunzi Chuoni hapo aliyejulikana kwa jina la Emmanueli Onesmo Ndanshau ameeleza kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakifeli chuoni hapo kutokana uzembe wa kutofanya mazoezi yatolewayo na waalimu wao madarasani na hata mazoezi ya vitendo
Habari na: Irene Mathias
Picha na: Joseph Richard
No comments:
Post a Comment