A.J.T.C
STARS WAENDELEA KUJIFUA KWA AJILI YA BONANZA JINGINE.
Mabingwa
watetezi wa bonanza la vyombo vya habari A.J.T.C STARS wameuomba uongozi wa
michezo katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha kurahisisha
vipengele vinavyowabana wachezaji chuoni hapo.
kutoka kushoto ni nahodha wa ajtc stars Bw.Stanly Lema akiwa na mwandishi wa habari Jackline Shayo katika moja ya darasa lililopo chuoni hapo mapema jana.PICHA NA JACKLINE SHAYO.
Akiongea
na mwandishi wa habari nahodha wa timu ya A.J.T.C STARS bwana Stanley Lema
mapema jana amesema kuwa licha ya wachezwaji wa timu hiyo kuwa wa ridhaa
kumekuwa na vipengele vinavyowabana na kuwafanya kushindwa kusakata kabumbu vizuri.
Bwana
Lema amevitaja vipengele hivyo kuwa nimuda wa kufanya mazoezi,mchakato mrefu wa
kupata vifaa vya michezo na idadi kubwa
ya wachezaji ambao wengine hawafanyi mazoezi.
Nahodha
Lema amemtaja mchezaji Samwel Paul kuwa ni mchezaji mwenyenye juhudi katika
kusakata kabumbu licha ya kuwa halipwi na hana vifaa binafsi vya michezo.
‘Amekuwa
ni mtu wa kujitolea kwa sababu anapenda mpira,so ni mfano wa kuigwa na
wachezaji wengine’ alisema Lema.
Lema
amezungumzia kabumbu iliyotimua vumbi katika kiwanja cha field force na kupigwa
kichapo cha 3-2 na kutolewa katika mashindano ya nani zaidi cup na mahasimu wao
Sombeti FC kuwa ni tatizo la marefarii au wachezaji wasiokuwa na ujuzi.
Stanley
alibainisha kuwa bonanza linalotarajiwa kufanyika septemba 12 mwezi huu
amewaomba wachezaji kujiandaa vyema kwa
mashambulizi na kuwaomba
mashabiki washangilie sana waende kwa wingi kushuhudia michuano a kuwaahaidi
mashabiki kuchukuwa undishi.
Mwandishi wa habari akiagana na Nahodha wa wanadinga wa ajtc stars mapema jana katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji arusha.PICHA NA JACKLINE SHAYO
No comments:
Post a Comment