HABARI NA ELINIPA E. TEMBA
Wananchi wameaswa kuwa na desturi ya kufanya usafi wa vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa U.T.I ambao umekuwa ukiwapata akina mama na watoto.
Hayo yamesemwa na daktari wa zahanati ya oljoro jijini arusha
Dk. Ayubu mashack katika mahojiano na mwandishi wetu hapo jana ambapo amesema
kuwa wanainchi wanatakiwa kuwa makini katika kuepuka swala la ugonjwa wa U.T.I
kwa kufanya usafi katika vyoo kila siku
Dk ayubu mashack
akizungumza n mwandishi wetu elinipa temba katika kufahamisha umma kuhusu
ugonjwa huu wa U.T.I mapema jana.Picha
na Selemani Juma Kodima
Dk Ayubu
alisema kuwa ugonjwa wa U.T.I ni ugonjwa unasababishwa na bacteria icolay
ambaye anasababisha uvinary tract infection
kwenye njia ya uzazi
Licha ya Dk
Ayubu kusema ni bacteria icolay aliweza kuzitaja dalili mbalimbali ambazo
mwanajamii anapoziona anaweza kujua kama ameshapata ugonjwa huu wa U.T.I
“Dalili kubwa ni chief complain
ambayo inapelekea maumivu makali wakati waaja ndogo na wakati mwingine maumivu chini ya kitovu ,homa kali hasa kwa watoto na
wakati mwingine kichefuchefu kwa watu wazima na kukojoa mara kwa mara “alisema Dk Ayubu
Ugonjwa huu
umekuwa ukiwashambulia sana wakina mama na watoto hali inayopeleke kuwa na
wagonjwa wengi wenye kupata ugonjwa huu wa U.T.I ambao wamekuwa wakikumbwa na
jangwa hili.
Dk Ayubu alisema yapo madhara ambayo mgonjwa wa ugonjwa huu
asipoutilia matibabu akaweza kukumbwa na hali ya utasa,hali inayopelekea
mwanamke kutoshika mimba hali inayopelekea wasiwasi kwa familia nyingi ambao
hawapo makini na ugonjwa huu
DK .Ayubu akizunguma kwa kina zaidi kuhusu dalili za ugonjwa huu wa U.T.I Picha na selemani juma kodima
Vilevile
amesema kuwa zipo juhudi nyingi ambazo
zinafanywa ili kuwapa jamii elimu ya
kuhusu namna ya kuepukana naugonjwa huu na kuwapa uelewa mpana wa ugonjwa
huu wa U.T.I japo matibabu yapo kwa
ugonjwa huu
Dk ayubu
amewashauri kuwa wanajami kuwa makini iwapo tu wanapoona dalili za ugonjwa huu
wa U.T.I ili kuepukana na madhara yanayotokana
ugonjwa huu
“wanajamii wakiona dalili yoyote wawe wepesi
kuja kwenye vituo vya afya kwa ajili ya
kupata matibabu ya ugonjwa huu wa U.T.I”Alisema Dk ayubu
No comments:
Post a Comment