Friday, 29 August 2014

Zimapp Yaonesha Mwanga

na KUNDAEL PHILLIP
        CHANZO BBC SWAHIL

Tabasamu la matumaini baada ya kupata ahueni ya Ebola
Hospitali moja nchini Marekani imewaruhusu wamisionary wawili wa kimarekani ambao walikua wakipata tiba kutokana na kuathiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, na imethibitishwa hawana athari kwa afya ya jamii.
Dr Kent Brantly na mtabibu mwenziwe Nancy Writebol ambao waliruhusiwa mapema wiki hii walipata maambukizi ya ugonjwa huo wakati wakiwasaidia wagonjwa wa ugonjwa huo nchini Liberia.
Kutokana na maambukizi walopata watabibu hao walipata maambukizi walipewa dawa ya majaribio ambayo haikuwahi kupewa binadamu hapo kabla,na dokta aliyekuwa zamu alishindwa kuthibitisha juu ya nafuu yao kama imetokana na dawa hiyo ya majaribio.
Kufuatia matokeo mazuri ya dawa hiyo ya majaribio dokta huyo wa zamu alijinasibu kuwa kituo chake kimejifunza namna bora ya kumsaidia mgonjwa wa bola na mazingira alimokuwamo, na kuahidi kushirikisha utaalamu huo kwa watabibu kutoka katika nchi za Kiafrica.
Nalo shirika la afya ulimwenguni W.H.O linaandaa mkutano utakao fanyika mwanzoni mwa mwezi huu katika mji wa Geneva nchini uswiss, utakaoangazia namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Takwimu za hivi karibuni zaonesha kwamba zaidi ya watu elfu kumi na tatu wamekufa kwa ugonjwa huo hasa kutoka katika nchi za Africa Magharibi Liberia,Sierra Leone na Guinea.

No comments:

Post a Comment