Friday, 29 August 2014

WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WAASWA KUJISHUGULISHA NA MAZOEZI YA VITENDO.




Mkufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Bw Adson Kagiye akiongea na mwandishi wa habari hiz ofisini kwake.
Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha ngazi ya Cheti na Stashahada wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wakifuatili jambo kwa makini.


Wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wameaswa kujishugulisha na mazoezi ya vitendo pamoja kuhudhuria darasani kwa wakati ili kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na Mkufunzi wa Taaluma ya Uhandishi wa habari na Utangazaji  Bwana Adson Kagiye wakati alipokuwa akiongea na mwanandishi wa habari ofisini kwake hivi leo.

 ''Wanafunzi walio wengi hawafanyi vizuri katika masomo yao jambo linalopelekea kufeli mitihani yao nakupata madaraja ya hali chini jambo linalopelekea kutopata cheti kizuri'' alisema Bw Kagie.

Aidha ameendelea kwakusema kuwa Chuo  kinao waalim Waliobobea  katika taaluma mbalimbali ikwemo ya uandishi wa Habari na utangazaji  pamoja na ualimu wa shule za awali na ile ya secretari

Pia ameongeza kuwa Chuo kina  studio nzuri na za kisasa za kurekodia vipindi vya Redio na Televishion hali ambayo itawafanya Wanafunzi hao kuwa na uzoefu katika usomaji wa habari pamoja na vipindi mbalimbali vya Redio na Televishen.

Vilevile amesema kuwa  kutokana na Wanafunzi kutofahamu vizuri Lugha  ya kiingereza kumechangia pia kutokufanya vizuri katika mitihani yao  hivyo amajipanga kuleta waalimu  kwa ajili ya mafunzo ya muda kwa Lugha ya Kingereza.

 Pamoja na hayo ameendelea kwa kusema kuwa wanafunzi ambao awajatimiza alama za kujiunga na chuo hicho watapewa kozi ya mda mfupia ya miezi kadhaa na ndipo watakapo jiunga na fani ya Uandishi wa Habari chuoni hapo.


Nae mmoja wa wanafunzi Chuoni hapo aliyejulikana kwa jina la Emmanueli Onesmo Ndanshau  ameeleza kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakifeli chuoni hapo kutokana uzembe  wa kutofanya mazoezi yatolewayo na waalimu wao  madarasani  na hata mazoezi ya vitendo

Hatahivyo Bwana  Ndanshau memalizia kwa kuwashauri Wanafunzi wenzake kuongeza bidii katika masoma kwa ajili ya kujenga elimu bora, Vilevile amewasisitiza Wanafunzi hao kuitumia Elimu ya Ujasiliamali Inayotolewa Chuon Hapo kwani itasaidia katika mambo mbalimbali  yakiwemo ya kujiajiri.HABARI  NA  WINLADY  JOHANESS  MBESERE

No comments:

Post a Comment