Tuesday, 12 August 2014

VAN GAAL AENDELEZA MARAHA MAN UNITED, YAICHAPA 2-1 VALENCIA

Na Stanley lema

KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuwapa rajaha mashabiki wa Old Trafford baada ya Manchester United jana kuifunga Valencia mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki.

Shujaa wa leo: Fellaini (wa tatu kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi


Sifa zimuendee Marouane Fellaini aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90 na ushei katika mchezo ambao, Wayne Rooney alikosa penalti kipindi cha kwanza iliyookolewa na Diego Alves.

United ilitangulia kupata bao kupitia kwa Darren Fletcher dakika ya 49 kabla ya Rodrigo kuisawazishia Valencia dakika ya 71.

Kikosi cha Manchester United: De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Young, Fletcher, Herrera, James; Mata; Rooney, Hernandez

Valencia: Alves; Barragan, Vezo, Otamendi, Gaya; Parejo, J. Fuego, Andre Gomes; Feghouli, Alcacer, Rodrigo



 Marouane Fellaini akiifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Valencia

Chanzo Binzuberi.bloggspot.comruwenzoriclass.blogspot.com

No comments:

Post a Comment