Na Stanley Lema
Mashindano ya kombe la mbuzi
yaliyopewa jina kama Nani zaidi Cup yanayoendelea kutimua vumbi kwenye viunga
vya Fid Force kwa Mworombo mkoa Arusha yamekuwa na taswira tofauti hadikufikia
sasa.
Mashindano hayo yaliyo anzishwa na
wadau wapenda soka maeneo hayo ya kwa Muorombo yamekuwa yakuvutia kwa mashabiki
achilia mbali vipaji vinavyo onekana kwa kila timu ambayo ni mshiriki .
Kikosi cha timu ya soka
ya AJTC stars kikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wake
dhidi ya FFU FC kwenye mashindano ya Nani zaidi Cup. (Picha na Jimmy Minja)
Lengo kuu la mashindano nikuakikisha
amasa ya mpira wa miguu maeneo ya viunga vya kwa Mworombo inarudi na kuakikisha
vijana wa maeneo hayo kurudi na kuupenda mpira kama zamani.
Kikosi cha timu ya soka
ya FFU FC kikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza mechi yake dhidi ya AJTC
stars kwenye mashindano ya nani zaidi cup yanayo endelea uko kwenye dimba la
FFU. (picha na Charles Chami)
Nikweli zipo timu nyingi ambazo
zimeweza kuonesha kiwango kwa kutandaza soka safi tena la kuvutia kwa kiwango
cha juu na kusababisha ata wadau kuhisi malengo yao yanaelekea kufanikiwa.
Nikweli wadau walioanzisha mashindano
hayo waliweza kufanikiwa kurudisha amasa kwa upande wa mashabiki na timu wa
shiriki ,nje ya hayao mashindano hayo yamekuwa na miguno ya hapa na pale kwa
timu wa shiriki kutokana na kuto tendewa aki kwa namna moja ama nyingine.
Swala la waamuzi kwenye mashindano
hayo limekuwa swala la kupigiwa kelele kila kukicha timu zinapo shuka dimbani
huku nyingine zikiwa zinalala mika kuwa kuna upangaji wa matoko ndani yake.
Mwenyekiti wa
mashindano ya Nani zaidi Cup Hassan Hatibu maarufu kama( Master) akizungumza na
mwandishi wa habari (kulia) kwenye uwanja wa ffu kwa mworombo mkoa ni
Arusha.Picha na Romana Chuwa.
Maneno haya yanaweza ya siwe na maana
kwa wapenda soka wakiweka kigezo kuwa mashindano hayo awajapata kuwaweka
marefari wenye hadhi ya kimataifa.
Pia zipo baadhi ya timu ambazo
zimeweza kuchanganya damu na kuwapa na fasi baadhi ya wachezaji chipukizi,
wachezaji wazawa ila zipo timu ambazo zimeweza kuwapa nafasi wachezaji wa
kukodishwa na hata wale walio wahi kucheza hata timu ya taifa kuonekana wa
kiskata kabumbu kwenye mashindano hayo.
Kiukweli mashindano haya ya nani
zaidi cup kwa namna moja ama nyingine yamekosa mpangilio kwenye upande wa
waandaji kwa kukosa kuweka sheriana na taratibu kwa kila timu wa shiriki.ruwenzoriclass.blogspost.com
No comments:
Post a Comment