Tuesday, 12 August 2014

KOCHA WA AJTC QUEEN AWASHUKURU TASWA

Na Winfrida James

Kocha wa kikosi cha timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha (AJTC) marufu kama AJTC Queen Bi Mercy Rodricky amewashukuru uwongozi wa Taswa kwa kuweza kutimiza ahadi waliyo waaidi.

Kocha uyo ambaye Timu yake hiyo ya netball inashikilia ubingwa wa bonanza la waandishi wa habari mkoani Arusha baada ya kunyakua na kuaidiwa kupewa seti moja ya jezi tofauti na zawadi waliyopokea kama mshindi wa kwanza .


Kocha wa timu ya netboll ya chuo cha uandishi wa habari arusha Bi Mercey Rodric (kulia) akizungumza na mwandishi wa habari hi hapo jana

Bi Mercy aliwashukuru Taswa badaa ya kupokea seti moja ya jezi za rangi ya blu na michirizi meupe kwa pembeni huku akidhihirisha furaha yake kwa kuwambia twasa daima wao watakuwa washindani wa kudumu kila litakapo tokea bonanza lolote ambalo wao wataalikwa .

Pia akusita kuwa shukuru wachezaji wa Timu yake kwa kuonesha juhudi pindi wakiwa mazoezini nakujituma wanapokuwa kwenye mechi na amewaaidi wa chezaji wake kuwa jezi walizo pewa azita tumika sehemu yoyote zaidi ya mchezo huo wa netball.

Bi Mercy ambaye pia alikuwa mchezaji mstafu wa timu hiyo amesema changamoto anayonayo mkabili ni ukosefu wa viatu kwa wachezaji pamoja na ubovu wa kiwanja cha kufanyia mazoezi.


Pia alitoa wito kwa wachezaji wa Timu yake kuzidisha kufanya mazoezi na kuweza kuendelea kugawa dozi kila watakapo shusha mguu kwenye viwanja nikugawa dozi ili zawadi zizidi kumiminika kwenye Timu yao. ruwenzoriclass.blogspot.com

No comments:

Post a Comment