(Zuhura Omary akisoma taarifa ya habari) |
NURDIN RAJABU, ARUSHA.
Wanafunzi wa darasa la manyara katika chuo cha uandishi wa
habari na utangazaji Arusha, wameuomba uongozi wa chuo hicho kutatua changamoto
mbalimbali zanazowakabili wanafunzi pindi wakiwa katika wiki ya habari.
Wanachuo hao wameyabainisha hayo wakati Ruwenzori blog
tulipowatembelea chuoni hapo wakiwa katika wiki yao ya habari ambao ni
utaratibu uliwekwa na chuo hicho kwa wanafunzi ambao wanakaribia kumaliza elimu
ngazi ya cheti au stashahada.
Joseph Samwel ambae ni mwanafuzi wa darasa hilo alisema
“Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni pamoja na kukatika umeme mara kwa
mara na kuisha kwa luku kwasababu unakuta umejiandaa toka nyumbani na kipindi
chako tena kwa muda unaotakiwa lakini ukifika studio unakuta hamna umeme hii
inakatisha tamaa sana tunaomba uongozi wa chuo utafufe jibu la hili suala ili
madarasa mengine wakifikia hatua hii wasipate tabu kama sisi”
(Joseph Samwel ambae ni mwafunzi wa darasa la manyara akielezea hisia zake juu ya wiki ya habari chuoni hapo.picha na ruwenzoriblog ) |
Nae Alex Mwenda ambae
pia ni kiongozi wa darasa hilo na Gilbert Johansen kwa pamoja walielezea
changamoto za kukosa ushirikiano baina yao na kwa wakufunzi pia gharama kubwa
za kutafuta habari mitandaoni kwasababu hutumia pesa zao wenyewe. “Mimi napewa
sh 2000 kila siku napewa nauli ya kupanda daladala sh. 800 na 1000 kwaajili ya
kula hiki ndio mzazi wangu anachoweza lakini nikija huku chuoni natakiwa nipate
pesa nyingine kwaajili ya kuingilia mtandaoni, wakati mwingine huwa naacha kula
mchana ili kufanikisha tu masomo yangu kama kuna jinsi ambayo uongozi wa chuo
unaweza kufanya kama kuweka huduma ya internet chuoni itakuwa vizuri”
alibainisha Gilbert Johansen.
(kutoka kushoto ni mwandishi wa blog hii Nurdin Rajabu na anaefuatia upande wa kulia ni Bw. Gilbert Johansen mwanafunzi toka darasa la manyara picha na ruwenzoriblog) |
Tulipowaaambia wanafunzi hao watoe mapendekezo ninikifanyike
walisema“Tunaomba uongozi wa chuo uboreshe mfumo wa uendeshaji vipindi chuoni
hapa ili kuoneza hamasa zaidi ya wanafunzi kuingia studio kujifunza, na luku
ikiisha inunuliwe mapema au chuo kiweke jenereta najua inawezekana kama
wanania” alisema mwanafunzi wa darasa hilo Zainabu Yusuph.
(Zainab Yusuph akimwelezea mwanahabari wetu jambo fulani wakati wakizungumzia juu ya wiki ya habari picha na ruwenzoriblog) |
Darasa la manyara ambao ndio mabingwa wa utangazaji chuoni
hapo kwa mwaka 2014 wameanza mitihani
yao ya mwisho jumatatu ya tarehe 11/08/2014 waliingia chuoni hapo 05/08/2013
wakiwa jumla wanafunzi 20 na wanatarajia kumaliza ngazi ya cheti 15/08/2014 na
idadi yao ikiwa ni 14 peke yake baada ya hao wengine 6 kuacha masomo kwasababu
mbalimbali kama magonjwa na wengine kubadili fani na kusomea mambo mengine.
(baadhi ya wanafunzi wa darasa la manyara wakiwa makini kuandaa vipindi mbalimbali muda mfupi kabla ya kuingia studioni kama ruwenzoriblog ilivyowakuta picha na ruwenzoriblog) |
(Alex Mwenda ambae ni kiongozi katika darasa la manyara akiwa katika mazoezi ya vitendo kutangaza katika wiki ya habari ya darasa lao picha na ruwenzoriblog) |
No comments:
Post a Comment