CHANZO BBC. HABARI NA ELINIPA TEMBA
Wanajeshi wa serikali ya Iraq
wanasema kuwa wamelikabili shambulizi moja la wanamgambo katika kiwanda
kikuu cha mafuta katika mji wa Beiji, na kuwaua wanamgambo kadhaa.
Kiwanda hicho kilichopo kazkazini mwa Iraq
kimekuwa eneo la tukio la mapigano kadhaa kati ya vikosi vya serikali na
wanamgambo katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita.Vyombo vya habari vya kikurdi vinasema kuwa miongoni mwa wale waliouawa ni maafisa wa kikosi cha kulinda amani cha kikurdi ,Peshemerga.
Wapiganaji hao wa kikurdi waliuteka mji huo wenye utajiri wa mafuta mnamo mwezi Juni baada ya jeshi la Iraq kutoroka likihofia mashambulizi ya wapiganaji hao wa ki-sunni.
Wakati huohuo bomu jingine limelipuka katika mji wa Erbil,ambao ndio mji mkuu wa jimbo la wakurdi,ikiwa ni tukio la kushangaza kwa kuwa ndio eneo lenye utulivu nchini Iraq.
Awali mlipuaji wa kujitolea muhanga aliwaua takriban watu wanane mjini Baghdad karibu na makao makuu ya ujasusi.
No comments:
Post a Comment