Thursday, 28 August 2014

RONALDO AFUNGUKA KUHUSIANA NA URAFIKI WAKE NA MESSI

Habari na Seif  Baruti



Kwa mara ya kwanza mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na Lionel Messi
SOMA ZAIDI  .......na kusema anamheshimu hasa juhudi zake za kutaka mafanikio kama mchezaji pamoja na klabu yake ya Barcelona.


SWALI. Baada ya miaka mitano sasa na Real Madrid, umechoka kulinganishwa na Messi au umejifunza jambo?
JIBU. Ni sehemu ya kazi tu kama vile ambavyo kwenye mashindano ya langalanga (Formula 1), watu wanafananisha kati ya Ferrari na Mercedes. Haya yamekuwa maisha yangu hapa Madrid, lakini najua mambo yanabadilika na hata nilipokwenda Manchester kulikuwa na mengine tofauti.
SWALI. Kumekuwa na taarifa kwamba uhusiano wako wewe na Messi nje ya mpira umekuwa si mzuri?
JIBU. Si kweli, sisi ni marafiki, ni marafiki kazini. Binafsi sina rafiki nje ya mpira, pia sina urafiki na Messi nje ya mpira. Anajitahidi kufanya makubwa katika klabu yake na timu ya taifa, sawa ninavyofanya mimi. Tunachezea timu zenye upinzani mkubwa na huenda ushindani huo unafanya watu wayakuze hayo mambo.
SWALI. Unafikiri wewe na Messi, siku moja mtakutana, mkae na kuanza kujadili haya yaliyotokea huku mkiangua vicheko kwa furaha?

JIBU. Nafikiri inawezekana, soka ni mchezo wa furaha, soka ni kitu kikubwa na unaweza kuufananisha na saa. Ndiyo maana nashauri kuwaangalia wapinzani kwa jicho la mafanikio na kukubali wanachofanya kwa vile ni kitu kizuri.

No comments:

Post a Comment