Mkulima wa mboga jijini Arusha
Bw;Athumani Idd akizungumza na mwandishi wa habari kuhusu faida zinazotokana na
kilimo cha mboga {picha na Olimpia Mallya}
Na;AULERIA GODFREY
ARUSHA
Wakulima wakilimo cha mboga Jijini Arusha wameaswa kutumia mbinu za kitaalam ili waweze
kunufaika na kulimo hicho.
Hayo
yamesemwa na mmoja wa wakulima Bw;Athumani Idd alipokuwa akizungumza na
mwandishi wa habari hapo jana kuhusu mbinu anazotumia katika kilimo chake na
namna anavyonufaika na kilimo hicho.
Ameeleza
kuwa wakulima wengi hawana elimu ya kutosha juu ya kilimo cha mboga ikichangia
kukosekana kwa pembejeo za kilimo ambazo
zingewasaidia kupata mazao bora ambayo yangesaidia kuwainua kiuchumi na
kuondokana na umaskini.
Akizungumzia
juu ya changamoto anazokumbana nazo katika kilimo ni pamoja na ukosefu wa
dawaza kuzuia wadudu,maji wakati wa kiangazi na soko la mboga kupolomoka kwa
asilimia kubwa kwa wakati wa masika.
Hata hivvyo
ameongeza kuwa wataala wa kilimo cha mboga wamekua wakijitaidi kutoa semina
mbalimbali kila siku ya jumamosi juu ya utayalishaji wa vitalu, upandikizaji wa
mbegu pamoja na utunzaji wa mboga
‘’watu wengi
wamekuwa wakizani kilimo ni kigumu, hakina faida na kinawapotezea muda si kweli
kwasababu mimi kimeniinua’’
Amezitaja
faida anazozipata kutokana na kilimo ni pamoja na kujenga,kusomesha na
kuendeleza miladi mbalimbali kama vile ufugaji na biashara ndogondogo.
Hata hivyo
Bw; idd ametoa wito kwa watu mbalimbali juu ya kilimo cha mboga na kuwataka
waache kukaa katika makundi na kusema kuwa kilimo hakinafaida kwao.
Ameiyomba
serikali kutoa semina mbalimbali kwa ajili ya kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo
kuwapa pembejeo na kuapatia elimu juu ya matumizi ya pembejeo hizo ili kujikimu
kiuchumi na kimaisha.
No comments:
Post a Comment