Sunday, 13 July 2014

MATOKEO YA MECHI KATI YA BRAZIL NA UHOLANZI

20140713-101157-36717149.jpg
NA
 NURDIN PALLANGYO
Hatimaye michuano ya kombe la dunia inafikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina, wakati usiku wa jana mshindi wa 3 wa michuano hiyo aliamuliwa kwa mechi kati ya Uholanzi vs Brazil.

Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa wa nchi hiyo, Brasilia, uliisha kwa matokeo ya ushindi wa 3-0 kwa Uholanzi, kikiwa kipigo cha pili cha Brazil ndani ya juma moja tangu walivyopokea kipigo cha magoli 7-1 kutoka Ujerumani.
Magoli ya Uholanzi yalifungwa na Van Persie, Blind na Georginio Wijnaldum.
Wakati kocha wa Uholanzi Louis Van Gaal akielekea Manchester United, kocha wa Brazil Luis Fellipe Scorali amesema pamoja na kuvurunda kwa Timu yake lakini hawezi kujiuzulu na hatma yake anaiacha mikononi mwa waajiri wake shirikisho la soka la Brazil.20140713-101224-36744905.jpg

No comments:

Post a Comment