NA
NURDIN PALLANGYO
Utafiti kutoka katika jarida la Lancet unaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya watoto ambao wamepewa chanjo hiyo wamepata ulinzi dhidi ya
ugonjwa huo.
Nusu ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo vinavyotokana na mbu.
Wataalam wanasema ingawa utafiti umekuwa ni wa muda mrefu wameahidi chanjo ya ufanisi mkubwa na muhimu ili kufanikisha lengo lao.
Kwa sasa hakuna tiba ya kuzuia homa ya dengue ugonjwa ambao unaathiri zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka.
Katika utafiti wa awali wa chanjo hiyo, watafiti kutoka vituo vitano katika bara la Asia waliwatibu watoto 6,000 wenye umri kati ya miaka miwili na 14.
Chanjo hiyo pia ina manufaa katika aina nyingine za magonjwa, na inapunguza idadi ya watu wanaohitaji matibabu katika hospitali kuanzia asilimia 80 ya kesi ya homa ya hemorajiki ambayo imekuwa ikitishia maisha ya watu.
No comments:
Post a Comment