Thursday, 3 July 2014

NEWS:RAISI KIKWETE ASIFIA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI



  Na Tumaini sylvester              
                                       Mh Jakaya Mrisho Kikwete

Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh Jakaya Mrisho Kikwete  amesifia uhusiano mzuri ulioko
kati ya nchi ya tanzania na nchi ya Africa kusini.

Hayo ameyasema mwishoni mwa wiki wakati akiwa anaagana na balozi wa Afrika kusini nchini mh Thanduyise henry chilinza ambaye amemaliza muda wake wa uongozi hapa nchini na anarejea nyumbani kwao

Aidha raisi kikwete amesema nivyema kwa nchi ya Afrika kusini kuendelea kuonyesha uongozi mzuri  katika
ukanda wa kusini mwa bara la afrika kwani inaendeleza lengo lake la kihistoria

Katika hatua hiyo raisi kikwete amesifia mchango wa afrika ya kusini katika kuonyesha mchango wake kwa utulivu ulioko kusini mwa afrika na kusema anatambua mchango wa nchi hiyo katika kutekeleza hilo

Kwa upande wake balozi chillinza amemshukuru raisi kikwete kwa kumuunga mkono wakati wa uwakilishi wake na hivyo kumsaidia kutimiza majukumu yake ya kibalozi hapa nchini.
        "namshukuru sana muheshimiwa raisi kwa ushauri na maelekezo yake ya kiuongozi wakati wa utumishi
          wangu katika taifa hili la tanzania na bila kunisaidia pengine kazi yangu ingekuwa ngumu zaidi".

No comments:

Post a Comment