Wakazi
wa kata ya sombetini kitongoji cha ngusero mtaa wa majengo mapya
wameomba na kuishauri mamlaka ya maji safi na maji taka jijini arusha auwasa
kushughulikia miundo mbinu ya mabomba yaliyo pasuka eneo hilo.
maji yakitiririka kutoka katika mabomba yalipasuka Ngusero |
Mabomba hayo yanayo leta athari katika barabara
za mitaa hiyo ikiwamo kuchimba mifereji midogo midogo na pia upotevu wa maji
unao sababisha wakazi hao kukosa maji wakati mwingine.
Mmoja wa wakazi hao bwana lazaro mollel aliomba na kushauri
mamlaka hiyo kutupia macho miundo mbinu yao ya sehemu tofauti tofauti nasio
eneo hilo pekee ili kuepuka hasara
zinazo weza kujitokeza kutokana na upotevu wa maji.
Moja ya viongozi katika kitongoji hicho
aliyeomba kutotajwa jina wala kupigwa picha alisema``sisi viongozi wadogowadogo
hatuwezi kushauri chochote hata tuki shauri hatusikilizwi”
Aidhaa kitengo cha huduma kwa wateja cha
mamlaka hiyo kwa njia ya simu walisema``malalamiko ni mengi na tuna jitahidi
kurekebisha kadri tunavyo weza’’
mwandishi
Adolph shoo
No comments:
Post a Comment