Maji machafu yaliyotuama katika soko la Mbauda mkoani Arusha |
Uchafuzi wa mazingira katika soko la Mbauda mkoani Arusha yahofiwa
kuathiri afya za wafanyabiashara
na wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na soko pamoja na wateja wanaokwenda sokoni hapo kupata
mahitaji yao.
Soko
la Mbauda ni soko ambalo limechanganya wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo
wauza mitumba,wauzaji wa chakula maarufu kwa
ajina la mama lishe pamoja na wengine wengi.
Mfanyabiashara
mmoja katika soko hilo bwana Ombeni Sinde ameeleza kuwa ni muda mrefu sana
wamekuwa wakitoa maoni yao kwenye uongozi wa soko hilo pamoja na uongozi wa
serikali kuhusu swala la usafi katika soko hilo,swala ambalo linaonekana
kutopewa kipao mbele.``hili soko sisi tumeshalalamika sana hadi kwa viongozi wa
serikali lakini hamna kitu,hapa kuna harufu mbaya lakini ndo hivyo
tumeshazoea’’
Hata
hivyo katika soko hilo kumekuwa na madimbwi ya maji machafu yaliyosimama pamoja
na takataka chafu ambazo zimekuwa zikitupwa kiholelaholela pasipokuwa na
utaratibu hali ambayo inasababisha harufu mbaya hata kupelekea magonjwa ya
mlipuko.
Mmoja
wa wafanyausafi sokoni hapo ambae ameomba jina lake lisitajwe amesema kuwa
pamoja na mazingira kutoridhisha lakini wamekuwa wakijitahidi kufanya usafi ka
kwenye soko hilo.Lakini pia alisema kuwa wanafanya usafi katika mazingira
magumu sana kwani vitendea kazi ni vichache,pia ameomba kwa watu wote kuwa
wastaarabu kwa kutotupa taka hovyo na kuyajali
mazingira ili kuepukana na maradhi.
Wananchi
pia wameiomba serikali kuongeza jitihada ya kuongeza vitendea kazi ikiwa ni
kuweka sehemu maalumu za kutupia taka pamoja na kuweka faini kwa yeyote ambae
atakiuka sheria zitakazowekwa kwa ajili ya kutunza mazingira.
Kwa
upande wake mmoja wa viongozi wa soko hilo,ambae ameomba jina lake lisitajwe
amesema kuwa wamekuwa na jitihada za dhati katika kuhakikisha mazingira
yanakuwa mazuri.Hadi sasa wameajiri wafanyausafi ikiwa ni moja ya mpango wa
kuhakikisha wanaweka mazingira vizuri.Pia kuna mpango wa kuweka eneo maalumu la
kutupa taka sambamba na kuweka faini kwa mtu atakaekiuka taratibu
zitakazowekwa.
Na Mwandishi;
Yesaya
Mwambelo
No comments:
Post a Comment