Friday, 23 May 2014

Bei ya mafuta bado gumzo kwa waendesha bodaboda jijini Arusha.

 Kutokana na ongezeko la bei ya mafuta,wafanyabiashara waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wameshindwa kujikwamua kiuchumi.


Hayo yamesemwa na wafanyabiashara hao waendesha pikipiki waishio kata ya Olasiti Mkoani Arusha wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya suala zima la ongezeko la bei ya mafuta.
waendesha bodaboda eneo la olasiti jijini Arusha
Akizungumza kwa niaba ya wengine Bwana Allow Saidi  amesema kuwa kutokana na bei ya mafuta kuwa juu hadi wanashindwa kufanya kazi yao kwa ufasaha kwani hakuna abiria anayekubali kuongeza nauli.

Pamoja na hayo amefafanua kuwa wanapata kashfa nyingi kutoka kwa abiria kuhisiwa wizi,utapeli na kusemekana 
kuwa hawathamini utu wa mtu.


Akizungumza kwa niaba ya abiria wanaotumia usafiri wa bodaboda Bw.Fredrick Joseph wameiomba serikali inayohusika na Mamlaka ya Usafirishaji yaani  SUMATRA kushughulikia kiwango cha bei ya mafuta ili wapate kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo waendesha pikipiki wanapaswa kuwa  makini na kazi yao lengo ikiwa ni kupunguza ajali za barabarani . 

mwandishi
hosiana Mbise

No comments:

Post a Comment