Friday, 23 May 2014

wafanyabiashara waaswa kuwa wabunifu ili kuhimili ushindani!!


Wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama mama lishe waishio maeneoya Majengo jijini Arusha,wametakiwa kuwa wabunifu ili kujiongezea faida katika biashara zao.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo jijini Arusha
Hayo yamesemwa na mmoja wa  ya mama lishe hao Bi,Flora Palanjo wakati akizungumza na A.J.T.C  FM hii leo  asubuhi.

Bi,Flora amesema kuwa ubunifu wa wafanyabiashara ni mzuri kwani huwaongezea wateja wao na sio kuigiana biashara.

Aidha amesema kuwa kuna faida mbalimbali waanazopata kama vile pesa za kusomeshea watoto wao,kulipa kodi ya pango la nyumba pamoja na kujiunga na vikundi mbalimbali ili kutunza fedha zao na kukopa maarufu kama vikoba.

Sanjari na hayo Bi, Jerima Lukumayi miongoni mwa wafanyabiashara hao amewaomba wanawake kujiunga na vikoba hivyo ili waweze kuanzisha biashara yoyote lengo ikiwa ni kujikomboa kiuchumi.

Hata hivyo amesema vikoba hivyo huwakopesha wafanyabiashara hao pesa kwa riba ndogo akatolea mfano wa kukopeshwa kiasi cha shilingi milioni moja unarudisha kwa riba ya shilingi laki moja.

mwandishi
Mary Elias
www.ruwenzori.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment