Waendesha
bodaboda wa kwa murombo jijini
Arusha wamelalamikia serikal kutowapa
Ushirikiano
katika kazi zao pamoja na kutowapa ulizi wa kutosha katika kazi zao
Kama ilivyo
kwa waendesha magari
Waemesema
hayo jana walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari jana katika kituo cha
barabara mpya fidifose ambapo ndo kituo chao cha kuegesha pikipiki za abiria,pia
wamesema changamoto kubwa ambazo
wanakumbana nazo nipamoja na
kunyanganywa pikipik zao
Pia mmoja wa
madereva hao aliejitambulisha kwa jina
Girlibet Mallya amesema baadhi ya abiria wakiwachukuwa wanata kuendesha
pikipiki wenyewe kitendo ambacho kinapelekea kuaribika kwa pikipiki kwani
awapomakini wakati wakuendesha wanajali masilai yao binafsi
''Kusema kweli kazi yetu ni ngumu na inaitaji
mtu kuwa mvumilivu kwasababu
ina vikwazo vingi mbali na hayo tumekuwa wakupata ajali mara kwa mara na
wenzetu wengi wamepoteza maisha tena wakiwa na umri mdogo;alisema Gilibert''
Mbali na
hayo madereva hao wamesema changamoto nyingine katika kazi zao bara bara zinazo
ingia katika makazi ya watu ni mbovu
kitendo ambacho kinapelekea wao kushindwa kufanya kazi kipindi cha mvua.
Pamoja na
hayo wamesema kuwa nauli wanazo pokea ni ndogo ukilinganisha na umbali wanao
mpeleka mteja hivyo wanashindwa kumudu garama za mafuta.
Madereva hao
wameitaka serikali kuwapa ushirikiano wa kutosha na kuwasaidia kutatua
changamoto zinazo wakabili ili kuwasaidia kuokoa maisha yao hasa wanapo kumbana
na majambazi wanao wateka nyara na kuwanyanganya
pikipiki zao.
HABARI NA NDETANISWA PALLANGYO NA ABDUL KAREEM
No comments:
Post a Comment