Kiongozi wa mabweni ya Oysterbay ( Kushoto )katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC)Bw.Edger Kisela akitoa ufafanuzi juu ya matatizo wanayokutana nayo katika mabweni hayo ( Kulia )Ni Suzane Chedy mwandishiwa blog hii.( Picha na Aziz Mwinuka )
Na.Suzane Chedy.
Rai imetolewa kwa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa
habari na utangazaji Arusha ( AJTC ) Kuzingatia suala nzima la usafi kuanzia
kwenye mabwani na chuo kwa ujumla ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na
uchafu.
Wito huo umetolewa na kiongozi wa mabweni ya
oysterbay katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bwana Edger Kisela
wakati akizungumza na mwandishi wa Blog hii Suzane Chedy.
Asema wanafunzi wengi wahapendi kufanya usafi kwa
sababu ya uvivu na kupuuzia maagizo yanayotolewa na viongozi wa mabweni hayo.
Bwana Kisela amesema kuwa upungufu wa vifaa vya kufanyia usafi pia limechangia kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa mabweni hayo kutojitolea kufanya usafi.
Kiongozi wa mabweni ya Oysterbay ( Kushoto )katika chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC)Bw.Edger Kisela akitoa ufafanuzi juu ya matatizo wanayokutana nayo katika mabweni hayo ( Kulia )Ni Suzane Chedy mwandishiwa blog hii.( Picha na Aziz Mwinuka )
No comments:
Post a Comment