Kushoto ni Eliamin Mchome,mhasibu wa JBC Akihojiwa
na mwandishi wa blog hii Catherine Prosper mapema leo
katika ofisi za JBC..PICHA NA SAMWEL PAUL
Eliamin Mchome,Mhasibu wakikundi cha uandish
wa habari na utangazaji[JBC]..PICHA NA SAMWEL PAUL
Habari na CATHERINE PROSPER,
Muhasibu wa
chama cha uandishi wa habari na utangazaji [jbc]
Eliamini
Mchome amezungumzia changamoto ,faida,hasara,pamoja na mafanikio
waliyopata tangu kuanzishwa kwa chama
hicho mnamo mwaka 2012 hadi kufika sasa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika eneo la chama amesema wamepata faida nyingi
pamaja na mafanikio makubwa kutokana na chama chao ikiwemo kuanzishwa kwa
mgahawa wa chama chao unaotoa huduma mbalimbali za chakula pamoja na vinywaji
“tunapata
fedha kutokana na mgahawa ,tunaweza kulipa wafanyakazi pamoja na kupata faida
inayoendelea kukuza mfuko wa chama”Alisema mchome
Amesema
chama kimefanikiwa kufikia moja ya malengo kiliyojiwekea yakutoa waandishi na
watangazaji bora watakaoweza kupambana na soko la ajira pindi wamalizapo masamo
yao ,na miongoni mwa wanafunzi wa chama hicho walioajiriwa na vyombo mbalimbali
vya habari ni Beatrice Shayo,Mohamadi Amad,pamoja na Beatrice moses.
Pamoja na
mafanikio tuliyonayo pia tunakumbana na changamboto mbalimbali ikiwemo
kukosekana kwa mwitikio miongoni mwa baadhi ya wanachama tofauti na hapo
awali,ambapo wanachama walikuwa chachu ya kupatikana kwa wanachama wapya
“kukosekana kwa mwitikio
kunatokana na wanachama wengi kuhitimu masomo yao na chama kubaki na wanachama
wachache”Amesema muhasibu huyo.
Amemalizia
kwa kuwataka wanachama kurudisha mwitikio wao ili kufikia malengo waliyojiwekea
katika chama ,pia wanawakaribisha wanachama wapya kujiunga na chama
hicho,pamoja na kuungwa mkono katika biashara yao ya mgahawa.
No comments:
Post a Comment