Baadhi ya wafanya biashara wadogo wadogo wa soko la
Mbauda Mkoani Arusha wameiyomba serikali
kuweka bei moja kwa wauzaji wa viazi vya jumla.
Pichani; Moja ya chakula kitokanacho na viazi |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema serikali
inapaswa kuweka bei moja ya viazi kwa wafanya biashara wa jumlaa kwani huwa
inabadilika siku hadi siku
Mmoja wa wafanya biashara hao, Bw. Fami Hamisi
alisema tunashindwa kuendesha biashara zetukwani bei ya viazi huwa haitabiliki
kila wakati inazidi kupanda.
Pichani; Bwana Fami Khamiakiongea na mwanahabari |
“Tunanunua viazi kwa bei ya juu sana
gunia wanatuuzia shilingi elfu kumi na mbili tena viazi vyenyewe ni vidogo sana
hakuna faida yeyote tunayopata”alisema Hamisi.
Bw,
Hamisi aliendelea kusema kuwa, gharama
inavyozidi kupanda inawalazimu na wao kuweza kupandisha, kwani hivi sasa debe
moja la viazi wanauza shilingi elfu kumi na mbili badala ya shilingi elfu kumi
na sado moja wanauza shilingi elfu tatu, tofauti na awali walikuwa wanauza
shilingi elfu mbili.
Nae
Bw, Issaka Ramadhani alisema kuwa, kutokana na viazi hivyo kutoka nchi jirani
ya Kenya ndiyo maana wanauziwa bei ya juu sana hivyo wanaiyomba serikali
kupitia wizara ya kilimo kuwekea mkazo kilimo cha viazi ili wanunue viazi
kutoka hapa nchini.
Aliendelea
kusema kuwa,anashukuru halmashauri ya manispaa
ya Arusha kwa kuwawekea kiwango kidogo cha cha kulipia kodi kwani kwa
siku huwa tunalipia kiasi cha shilingi mia tano.
“
Manispaa yetu imefanya jambo zuri sana kutuwekea kiasi kidogo cha ulipaji
ushuru kwani tunalipia shilingi mianne ya ushuru na shilingi mia moja kwaajili
ya usafi wa soko letu”
Pia
wameiomba serikali iweze kuwatafutia eneo kubwa na lenye ubora la kufanyia
biashara hususani kwa wauzaji wa viazi sokoni hapo kutokana na mabadiliko ya
hali ya hewa.
Habari na Seif Baruti / Salha Mustapha
No comments:
Post a Comment