Mwandishi wa habari kushoto Magreth chuwa akifanya mahojiano na mfanyabiashara maarufu kama mjasiriamali Salma mboya wakati akifanya shughuli zake za kimaendeleo.
Picha na:mpiga picha wetu
|
Wanawake nchini wametakiwa kuwa wawajibikaji katika shughuli
mbalimbali za kiuchumi ili kuondokana na hali ngumu ya maisha na tatizo la umasikini.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hapo jana salma mboya maarufu kama mjasiriamali
amesema njia pekee ya kuinua kipato na kuondoa umasikini ni kujishughulisha na
biashara mbalimbali ambapo yeye anapika chipsi na kuuza ndizi,samaki,pamoja na
viazi.
Pia amesema
biashara yake ni ya muda mrefu takribani miaka minne na biashara imemsaidia
mambo mengi kama vile kusomesha watoto wake,chakula mavazi pamoja na kumalizia nyumba
yake.
Ameendelea
kusema wakina mama wote wanatakiwa kijituma ipasavyo kibiashara hivyo waache
kukaa bure bila kufanya kazi kwa sababu mtu anatafuta umasikini mwenyewe hivyo
ili kudidimiza umasikini lazima watu wawajibike kwa bidii.
Salma
ameendelea kusema ukitaka kuwa na maisha mazuri lazima ujitume kwa bidii katika
kujishughulisha na kazi mblimbali kama vile kufungua migahawa,kuuza mchicha,na
shughuli mbalimbali za kibiashara ili kujikwamua kiuchumi.
Amemalizia
kwa kusema kuwa anawasihi wakina mama wanaokaa bure bila kujishughulisha na
shughuli yoyote wanaita umasikini na maisha yao yatazidi kuwa magumu
wasipofanya juhudi ya kufanya biashara.
Na Magreth chuwa
No comments:
Post a Comment