Wednesday, 13 August 2014

Vijana hapa nchini wameaswa kujishuhulisha na kuwa wabunifu

Kushoto ni mmiliki wa blog ya jimmcarte.com akizungumza na mwandishi wetu Rodasia Kimati(picha na Magreth Chuwa)

Vijana hapa nchini wameaswa kujishuhulisha na kuwa wabunifu wa
utafutaji,na kujitolea, kuweza kuondokana na umaskini.
Mmoja wa kijana wakitanzania Jimmy Minja ambae ni mmiliki wa blogi iitwayo www.Jimmcarte.com ameweza kubuni jinsi ya kijipatia kipato kwakutumia blog.

Ni kijana mwenye umri wa miaka 25 mzaliwa wa Kilimanjaro alipata wazo la kumiliki blogkwanzia akiwa katika mafunzo yake ya sekondari,alivutiwa na baadhi ya watu waliyoweza kumiliki blogi na kufanikiwa kimaisha
Ndoto zake zilifanikiwa baada yakujiunga na mafunzo ya chuo katika fani ya uwandishi wa habari na utangazaji katika chuo cha arusha journalisim traing college  ajtc aliweza kukutana na kijana mwenzake aitwae NOLNIZ,na aliweza kumtumia na kumwelekeza kuhusiana na blogi,pia aliweza kumsaidi kufungua blog na kuanza kumiliki blogi yake mwaka 2012
Pamoja na masomoaliweza kutenga muda wake vizuri nakufanya kazi yake ya kutuma habari katika blogi yake kama moja ya kazi za darasani kwanzia saa kumi jionimuda wa kutoka darasani hadi saa sita usiku anaweza kutuma habari katika blogi yake.
Pamoja na hayo kijana huyu amejiwekea malengo yake yakusaidia  wote wenye vipaji mbalimbali vya burudani ili aweze kuishi kupitia blog.
Licha ya kuwa na malengo,ameweza kukutana na changamoto nyingi kama vile watu wanakuja kumwomba awatengenezee skendo ambazo haziruhusu katika faani yake ya uwandishi wa habari changamoto nyingine ambayo inamsumbua  ni network yakitanzania bado ipo chini sana.

Kuna watu wanaishi kwa kutumiah hii mitandao yani kuwa na blog na maisha yao bado ni mazuri,wame weza kujenga na kupata pesa za kuwatosha ,alimaliza kwa kusema hayo.

                                                                   Bloger Jimmy Minja
Habari na Rodasia kimati


No comments:

Post a Comment