Mshindi wa mashindano ya taji la
Miss Asia Pacific World, May Myat Noe, amevuliwa taji lake akisemekana
ni mjeuri, hana hadhi na hastaili taji hilo.
.
May Myat Noe, mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka Burma, sasa anaripotiwa kutoweka na taji alilovikwa aliposhinda mwaka jana ,msemaji wa waliodhamini taji hilo anasema msichana huyo wa miaka 18 alitoweka baada ya kufahamishwa uamuzi huo wa kumpokonya taji hilo wiki jana.
Imefahamishwa kwamba waandalizi wa shindano hilo pamoja na mamake msichana huyo walitofautiana kuhusu usimamizi wake, Shirika lilioandaa shindano hilo, limesema kuwa Bi May alidanganya na kwamba hana heshima kwa waandalizi wa shindano hilo
waandalizi hao wanasema kukosa heshima kwake ni moja ya sababu za kumpokonya taji lake kadhalika shirika hilo lilisema kuwa msichana huyo, aliyekuwa amepata mikataba ya kufanya rekodi ya miziki pamoja na kuigiza, alitoroka na taji lake lenmye thamani ya dola 100,000.
Mamake May alionekana kutaka kumsimamia msichana wake, lakini chini ya masharti ya shindano hilo, mshindi anapaswa kusimamiwa na waandalizi.
Inadhaniwa kuwa bi May amekwisha rejea burma
Source , BBC SWAHILI
Na Jackline malecela
Source , BBC SWAHILI
Na Jackline malecela
No comments:
Post a Comment