Mawaziri wa Afya wajadili Ebola
habari na Jackline Shayo
Mawaziri wa afya kutoka nchi za
Afrika Magharibi wamekubaliana kuondoa upigaji marufuku wa safari za
ndege na ufungaji wa mipaka kwa nchi ziliathirika kutokana na ugonjwa wa
Ebola. Mawaziri hao ambao wamekutana mjini Accra, Ghana kupitia upya
mikakati iliyokuwa ikitumika kupambana na virusi vya ebola pia wametoa
ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari zao katika nchi
zilizoathirika.
Shirika la Afya la Afrika Magharibi lina wiki moja ya kuandaa hatua za kuchukua na kuandaa bajeti ili kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani na wadau wengine.
Mawaziri wote wa afya isipokuwa wale wa kutoka nchi zilizoathirika kutokana na ugonjwa wa ebola za Guinea, Sierra Leone, Liberia na Nigeria walihudhuria mkutano huo.
Waliobaki hawakuweza kuhudhuria kutokana na matatizo ya ndani na matatizo ya usafiri wa ndege ambao umesitishwa katika nchi zilizoathirika.
Mawaziri wa Afya wametoa ombi maalum kwa mashirika ya ndege kurejesha safari za ndege na kuendelea kuruka kwenda katika nchi zilizoathirika.
Hata hivyo wamesisitiza upimaji wa joto la mwili na kuhakikisha usafi wa mikono katika vituo vya kuingia na kutoka
chanzo;BBC
No comments:
Post a Comment