Mganga mkuu katika zahanati ya orjolo iliyopo mkoani
arusha,ametoa hamasa kwa wazazi na walezi kuzingatia umuhimu wa chanja kwa watoto kabla na baada ya kuzaliwa.
Haya yamesemwa na Dr Mathew mwingira wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi ofisini kwake
Dr Mwingira amesema kuwa ni vyema wazazi na walezi kuchunguza afya za watoto
hili kuwakinga na magonjwa nyemelezi hususa katika msimu huu wa mvua na
kuongeza kusema kuwa idadi kubwa ya wagonjwa ambao
wamefikishwa katika zahanati hiyo kwa msimu huu ni watoto kuanzia umri wa miaka 0-5 wakisumbuliwa na kifua (nimonia)
wamefikishwa katika zahanati hiyo kwa msimu huu ni watoto kuanzia umri wa miaka 0-5 wakisumbuliwa na kifua (nimonia)
kwenye picha ni mganga mkuu wa kituo cha afya oljoro bwana mathew mwingira |
Hivyo basi Dr Mwingira amewataka wazazi na
walezi kuhakikisha watoto wao wanawavisha mavazi mazito na kuepuka matumizi
yavyakula vya baridi au barafu
Hata hivyo mmoja wa wazazi ambaye hakutaka kupigwa picha,anaefahamika kwa jina la mama isiyaka amesema mwanae alisumbuliwa na kifua[nimonia] kwa siku mbili lakini anashukuru hali imebadiri baada ya kufika zahanati hapo
Mama isiyaka ameongeza kusema kuwa wazazi
na walezi kwaujumla wanatakiwa kujari afya zao na familia kwa kutunza mazingira
No comments:
Post a Comment