Wafanya biashara ndogondogo katika soko la kwamorombo kata
ya mbuga ya chumvi jijini arusha wameitaka serekali na uongozi wa soko hilo
kuharakisha ujenzi wa miundombinu sokoni hapo
Halihalisi katika soko la kwamorombo jijini arusha |
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wanapata
usumbufu mkubwa pamoja na wateja wao kwani wamekuwa wakifanya biashara zao
pembezoni mwa barabara jambo ambalo limekuwa likiwasumbua na kusababisha
mgogoro na askari wa jiji mara kwa mara
Aidha wamesema kufanya biashara zao pembezoni mwa barabara
inapelekea uchafu wa mazingira hasa nyakati za mvua ambapo kunakuwa na matope
pamoja na maji machafu yanayopita katika mitaro kutoka sehemu mbalimbali za
makazi ya watu
Kwa upande wake katibu kata wa mbuga ya chumvi katika eneo
hilo la kwamorombo ambaye hakutaka jina lake litajwe,Alisema kuwa miundombinu
ya soko hajakamilika ikiwa ni pamoja na umeme,uzi wa soko,vyoo na mahitaji
mengineyo ya soko hilo
Pia ameongeza kwa kusema bajeti kwajili ya ujenzi wa
miundombinu ya soko hilo imesha tegwa
ili kukamilisha ujenzi wa soko hilo kwa muda wowote ili kuepusha adha ya
uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na usumbufu kwa wafanyabiashara na wateja
wa bidhaa zao
Mwandishi
Richard Budala
No comments:
Post a Comment