ZAIDI ya Watu lakini tano (500, 000) Mkoni
Simiyu, wanakabiliwa na Njaa kutokana na kutopata Mvua, hali inayofanya
Mazao yao kukauka kwa sababu ya jua.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti ametoa agizo hilo Machi 18, mwaka huu ambapo amewataka
Wananchi wa Mkoa huo, wasiuze Chakula kidogo walichopata kwani hivi
sasa hali ni mbaya huku akiwaagiza Viongozi wa Wilaya kuhakikisha kuwa
wanadhibiti uuzwaji wa Chakula kwa baadhi ya Wananchi wa maeneo husika.
Wakielezea hali ya Chakula katika Kata
zao, baadhi ya Madiwani wa Mkoa huo wamesema hali ya Chakula katika Kata
zao ni mbaya kutokana na Ukame unaosababishwa na hali ya mabadiliko ya
tabia ya Nchi.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa amewaagiza
Wananchi wa Mkoa huo, kulima Mazao yanayostahimili Ukame, kama Mtama,
Viazi Vitamu na Kunde ili kuendana na Hali ya Hewa.
No comments:
Post a Comment