Ndugu wa waliopotea wameelezwa kuwa wakae tayari kupata habari mbaya
Zoezi la kutafuta ndege ya abiria yaMalaysia limeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu wa watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo.
Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, marambili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.
Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.
No comments:
Post a Comment