Kushoto mwandishi wetu Ellen bampale akifanya maojiano na mkuu wa kitengo cha nidhami mr; Christian Ndege mapema leo (picha na Agape Msumari) |
Wanafunzi wa chuo
cha uandishi wa habari na utangazaji
arusha waaswa kuwa na nidhamu ndani na
nje ya chuo hicho yameelezwa na mkuu a kitengo cha nidhamu Mr Christian Ndege mapema jana alipokuwa
ofisini kwake alisema wanafunzi wanatakiwa na nidhamu kwani nidhamu ni msingi
wa maendeleo na wao kama walezi wa wanafunzi hao wanatakiwa kuwalea ili kuwa
waandishi bora na mfano huko waendako.
Pia alisisitiza
kuwa chuo hakina lengo la kumuadhibu mwanafunzi yeyote ila ni kumfanya
mwanafunzi akae katika mstari . Akiongelea malalamiko ya wanafunzi kuhusu kuvaa
sare za chuo pindi wanapokuwa chuoni
alisema kuwa ni wajibu kila mwanafunzi kuvaa sare za shule pindi wanapokuwa
chuoni na nguo zenye staaha pindi wanapokuwa mazingira ya chuo.
mr; Christian ndege |
Mwisho kabisa
walitoa wito kwa wanafunzi walioko chuoni wafuate sheria za shule ili wawe bora
huko wanapokwenda na pia kwa wale wanaokuja kujiunga na chuo waamini kuwa
watakuwa bora pindi watakapotoka hapa lakini kwa wale wanaokuja chuoni basi
wamepotea na AJTC hapatawafaa. HABARI NA ELLEN BAMPALE
No comments:
Post a Comment