Tuesday, 12 August 2014

RONALDO AIONGOZA MADRID KUICHAPA SEVILLE MABAO 2-0 NA KUTWAA UBINGWA WA SUPER CUP.


Habari na Winfrida James


Capture
Wachezaji wa timu ya Real madrid wakishangilia baada ya kunyakua kombe la UEFA super cup hapo jana baada ya kuifunga FC Seville .



Cristiano Ronaldo amefunga mabao yote mawili yaliyoipa ushindi wa mabao 2-0 timu yake ya Real Madrid dhidi ya FC Seville kwenye mchezo wa UEFA Super Cup ulipigwa nyumbani kwa Gareth Bale Mjini Cardiff kwenye dimba la Millenium.



Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao hayo mbele ya mashabiki 33,500 na kuipa Real ubingwa huo kwa mara nyingine tangu mwaka 2002.mchezo huo pia ulihudhuliwa na kocha wa zamani wa Man Utd Sir Alex Ferguson



Real Madrid kwenye mchezo huo iliwatumia nyota wake iliowasajili msimu huu kiungo mjerumani Toni Kroos pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina James Rodriguez.
Nahodha wa timu hiyo Iker Casillas alikaa milingotini siku moja tu baada ya aliyekuwa mpinzani wake msimu uliopita Diego Lopez kujiunga na AC Milan ya Italia.

CHANZO NA Shaffidauda.blogspot.com.ruwenzoriclass.blogspot.com

No comments:

Post a Comment