Watu wenye silaha wamewaua raia kadhaa waliokuwa wamehifadhiwa katika
kituo cha Umoja wa Mataifa mjini Bor katika jimbo la Jonglei nchini
Sudan Kusini, katika mauaji yaliyoelezwa na waziri kuwa ni ya kulipa
kisasi.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power, alisema watu
wasiopungua 20 waliuawa jana, baada ya raia waliojihami kwa silaha
kuvamia kituo hicho cha Umoja wa Mataifa na kuanza kuwafyetulia risasi
raia wenzao kutoka kabila hasimu.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS, ulisema watu hao waliingia katika kituo hicho kama waandamanaji wa amani, wakiomba kuwasilisha waraka, lakini walivyoingia wakaanza kuwafyetulia risasi wakimbizi. Vikosi vya UNMISS vilijibu mashambulizi -- kwanza kwa kufyatua risasi hewani na baadaye mapigano makali yaliibuka kabla ya wapiganaji hao kukimbia.
Umoja wa Mataifa walaani
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephanie Dujarric alilaani shambulio hilo dhidi ya raia na kusema linachochea zaidi mgogoro wa kikabila, ambao umelichagiza taifa hilo changa kabisaa kwa zaidi ya miezi minne sasa.
"Shambulio hilo dhidi ya eneo ambako raia wanalindwa na Umoja wa Mataifa ni uchochezi mkubwa, katibu mkuu anazikumbusha pande zote kwamba shambulio lolote dhidi ya walinda amani halikubaliki, na ni sawa na uhalifu wa kivita.
Katibu Mkuu anatoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuchukua hatua zote kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, ulinzi wa maeneo ya raia nchini Sudan Kusini, na pia anatoa wito kwa pande zote kujizuwia na vitendo au matamshi ambayo yanaweza kuchochea hali zaidi," alisema Dujarric.
Maelfu wameuawa na zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makaazi yao tangu mapigano yaibuke mwezi Desemba kati ya wafuasi wa makamu wa rais alieondolewa Riek Machar na vikosi vitiifu kwa rais Salva Kiir. Vikosi hivyo pinzani vinatokea katika makabila hasimu, na hivyo kuongeza hatari ya ukabila katika mgogoro hu

No comments:
Post a Comment