Tuesday, 15 April 2014

SERIKALI YAAHIDI KUWASILISHA HATI YA MUUNGANO BUNGENI !!!



Mwenyekiti wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira akiwasilisha maoni ya Kamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo.
Mwenyekiti wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira akiwasilisha maoni yaKamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha ishirini na mbili cha Bunge hilo.


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaribu, Stephen Wassira amesema Serikali itawasilisha Hati ya Makubaliano ya Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba baada ya siku mbili zijazo.

Wassira ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita ya Bunge hilo ambazo zilikuwa zikijadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba, alitoa kauli hiyo leo baada ya kuzuka mjadala juu ya uwepo wa hati hiyo na kama ipo kwa nini haijawasilishwa kwa wajumbe wa Bunge hilo.
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo, kabla ya kuanza kutoa taarifa za wajumbe walio wengi na wachache juu ya majadiliano ya sura hizo.

 “Nataka kuwahakikishia Hati ya Muungano ipo tena ipo katika hali nzuri. Nataka kuhaidi kwamba hati hiyo itafikishwa katika Dola ya Jamhuri ya Muungano siku mbili zijazo,” 








 “Hii ni kweli, kwa vile mwaka 1964 Rais Julius Nyerere aliwawakilisha Watanganyika na Rais Abeid Amani Karume aliwawakilisha Wazanzibar wote katika makubaliano ya kuunganisha nchi zetu mbili.”
Wassira alisema kubadilisha hati ya muungano unahitaji kwanza kurudisha Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kisha kupitia kura ya maoni, uamuzi wa mfumo gani wa Muungano na kama ni shirikisho, basi viongozi wa Tanganyika na Zanzibar wajadiliane aina ya ushirikiano.Katika Kamati hiyo, Wassira aliwasilisha maoni ya wajumbe wachache ambao walipendekeza Muungano wa Tanganyik na Zanzibar uwe wa Shirikisho.Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Kamati Namba Saba ya Bunge hilo, kuhusu Sura ya Kwanza nay a Sita, ya Rasimu ya Katiba, Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngiwilizi aliwasisha maoni ya kamati yake, ambayo pia wajumbe wengi walipendekeza muundo wa Serikali Mbili na maoni ya wajumbe wachache walipendekeza Muundo wa Shirikisho lenye Serikali Tatu.

No comments:

Post a Comment