Chelsea vijana wa darajani Stanford, jijini London, wamewanyamazisha vinara wa ligi kuu ya England, Liverpool baada ya kuwachakaza mabao 2-0 katika uwanja wao wa Anfield.
Liverpool ikiwa imeuanza mchezo huo kwa kasi na
kwa dhamira ya kupata ushindi ilishuhudia jahazi lake likitota katika
dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.Liverpool hawakukubali kusalimu amri kwa wageni,kwani waliendelea kupeleka mashumbulizi ya hatari langoni mwa wapinzani wao wakiishia kwa kosa kosa. Liverpool wanapigania ubingwa wa ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza katika miaka 24 iliyopita.
Chelsea katika mchezo huo ilikuwa ikipewa nafasi finyu ya kuibuka washindi. Lakini ni Jose Mourinho aliyeibuka na kicheko, huku Brendan Rodgers akiugulia kipigo cha kwanza kwa timu yake tangu kuanza kwa mwaka huu.
Kwa ushindi huo sasa, Chelsea inaachwa pointi mbili nyuma ya Liverpool ambayo inaoongoza ikiwa na pointi 80, baada ya michezo 36. Msimamo wa timu hizo ni Liverpool pointi 80, Chelsea 78, Manchester City 74, itakuwa na pointi 77 iwapo itaifunga Crystal Palace katika mchezo wao, huku Arsenal ikichukua nafasi ya nne ikiwa na pointi 70. Manchester City na Arsenal zimecheza mechi 35 kila moja huku Liverpool na Chelsea zikiwa zimecheza mchezo mmoja zaidi.
BBC Swahili imehabarisha
www.irundemtumtumwire.blogspot.com
No comments:
Post a Comment